2 Januari 2016 - 19:15
Kuuwawa kishahidi Mbaharain mmoja na mashia wengine watatu katika walionyongwa leo nchini Saudia

Serikali ya Saudi Arabia asubuhi ya leo imemnyonga Mbaharain mmoja na mashia wengine watatu ikiwa ni miungoni mwa idadi ya watu walionyungwa leo pamoja na sheikh Nimr (kiongozi wa mashia nchini Saudi Arabia)

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari ya kuuwawa kwa sheikh Nimr Baqir Nimr na watu wengine 46 zimetolewa asubuhi ya Jumamosi katika hali ambayo mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mbalimbali dunia vikisambaza habari hiyo, ama baada ya kufanya uchunguzi mdogo katika majina ya watu hao walionyongwa kukafahamika ukweli wakuwepo watu wa mataifa mengine.
Miungoni mwa watu walionyongwa ni kijana akiwa na jina la Muhammad bin Faisal bin Muhammad Ashuyukh) ambaye ni raiya wa taifa la Bahrain kitu ambacho kimeleta mshangao kwa baadhi ya mataifa.
Kijana huyo alikamatwa katika maandamano ya amani nchini Bahrain dhidi ya utawala wa nchi hiyo na baadaye kuamishiwa nchini Saudi Arabia na leo kuwa katika idadi ya watu walionyongwa na utawala wa Saudi Arabia.
Hii ni katika hali ambayo watu wengi duniani wanaamini kuwa kuuwawa kwa kijana huyo wa Bahrain na utawala wa Saudi Arabia utakumbana na radi amali za jumui za kimataifa kwakuwa kijana huyo ameuwawa bila ya kuwa na hatia pia kuuwawa kupitia taifa lengine.
mwisho wa Habari/290